Logo Bunia info24

Ituri/Irumu : Mashirika yaki raia ya Walese Vonkutu ya hitaji ujio wa gavana jeshi Luboya N’kashama ku ipapasa hali ya usalama

Mashirika yaki raia kwenye usulutani ya Walese Vonkutu yame jutiya ku rudi Bunia kwake Luboya N’kashama Johnny, gavana jeshi wa mukoa wa ituri, baada ya ziara yake mutaani Mambasa tarehe 25 july mwakani bila ku wasili maeneo ya Luna kupitia komanda ili ajioneye hali ya usalama jisi ilivyo.

Soniau Malangayi, katibu wa Mashirika yaki raia ya walese vonkutu, alipendeleya gavana Luboya N’kashama Jonny aki safiri ndani ya mukoa wa ituri haswa kwa kipindi hiki cha hali ya dharura asitumiye ndege bali gari ili ajioneye hali halisi ilivyo.

Malangayi ame iambia Bunia-info24.com kwamba waasi wa ADF wa endeleya ku zunguka kyenyeji wilayani Walese Vonkutu bila ku sakwa na jeshi la jamuhuri yaki demokrasia ya kongo (FARDC).

Tukumbushe kwamba, raia waliyo kimbiya na kurejeya vijiji vyao kwenye barabara Komanda hadi Luna kweye mupaka na Kivu kaskazini wame rejeya komanda kulingana na ukosefu wa usalama baada ya vijiji vyao ku shambuliwa mara kwa mara na ADF.

Mwandishi : Prince Syaghenda

Trad : Magloire KAKULE

18 vues
Partager

Laisser un commentaire